Kibolongan

Kibolongan ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wabolongan kwenye kisiwa cha Kalimantan. Mwaka wa 2002 idadi ya wasemaji wa Kibolongan imehesabiwa kuwa watu 30,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibolongan iko katika kundi la Kiborneo-Kaskazini. Wengine wanaiangalia kama lahaja ya Kitidong au Kisegai.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search